HISTORIA YA MAISHA YANGU
Jina langu naitwa David mbwiga, nimezaliwa tarehe 22-5-1990 katika hospitali ya mgololo, wilayani Mufindi mkoani Iringa, ni mtoto wa nne katika familia yenye watoto wanne, baba yangu mzazi anaitwa Mr Jonasy mbwiga, mama anaitwa Mary mwamasangula, wao wamejaliwa kupata watoto wanne, kati ya hao wawili ni wanawake na wawili ni wanaume, mtoto wa kwanza ni stephen, akifuatiwa na dada martha, alafu dada Rehema na mimi ni wanne.
Nikiwa nina umri wa miaka mitatu wazazi waliamua kunipeleka shulen, japo kuwa nilikuwa nina umri mdogo pia akili yangu ilikuwa haijakomaa, sababu kubwa iliyo wapelekea wazazi kunipeleka shulen katika umri mdogo ni kuwa hakukuwa na mtu wa kubaki naye nyumbani, nakumbuka shule niliyopelekwa ilikuwa inaitwa mgololo nursery maalufu kama chekechea au shule ya vidudu.
Baadhi ya walimu wangu wa kwanza kabisa ninaowakumbuka kunileta mimi katika system ya elimu ni kama mwalimu lusalua, mwalimu sambali, mwalimu haule...nilipata magumu mengi sana katika mda wangu wa kwanza wa masomo, kwani sikufahamu umuhimu wowote wa masomo na mda mwingi sana sikupenda kukaa shuleni, na kitu kikubwa nilichochukia ilikuwa ni kuandika, lakini nakumbuka nilikuwa nina rafiki yangu ambaye alinizidi umri kidogo hivyo yeye ndiye aliyekuwa ananisaidia mimi katika kuandika, namkumbuka kwa jina alikuwa anaitwa Musa king`ala.
Nawashukuru saana walimu wangu wa chekechea kwani nilisoma pale kwa mda wa miaka miwili na baada ya hapo na mimi nilikuwa kati ya wanafunzi bora kabisa hivyo nilisonga mbele katika shule maarufu sana iliyoitwa shule ya awali,, pale nilikuwa nina marafiki zangu wakubwa sana kama edger nkigi, frank mtoka, yohani simalagase, ruben kilamiti leah nyakunga, getrude haule,.,.,.,.,.,.,.n.k
Maisha yangu ya awali hayakuwa magumu kabisa kwa sababu ya msingi mzuri niliowekewa na walimu wangu wa mwanzo, ila nilikuwa kati ya wanafunzi waliofanya vizuri sana. baadhi ya walimu ninaowakumbuka ni mwalimu msewa, mwalimu ndeme, mwalimu kobelo, mwalimu eliza
Namshukuru Mungu mnamo mwaka 1998 nilianza darasa la kwanza na walimu wangu walikuwa ni mwalimu nyinge, mwalimu mbwaga, mwalimu kiliwa,. namshukuru Mungu maisha yangu ya primary yalikuwa mazuri kwani niliweza kufanya vizuri katika masomo, japo nilipata magumu mengi sana ya darasani, kama vile uonevu kutoka kwa wanafunzi wakubwa kiumri,, vile vile kuna dada ambaye yeye alikuwa vizuri sana darasani hivyo aliweza kutoa changamoto sana kwani mara nyingi sikufurahia kabisa kupitwa na mtoto wa kike katika masomo,, popote ulipo dada Deokara muhina respect kwako.
Walimu wangu kwa ujumla wa primary ninaowakumbuka ni mwalimu mawala, mwalimu Makota, mwalimu mshongo, mwalimu mchimae, mwalimu mwenduganga, mwalimu mfumya, mwalimu mwakalinga, mwalimu mwamasangula,,.,.,.,.,.,.,,,.,
Kutoka moyoni nawashukuru walimu wangu kwa kunipa msingi mzuri katika masomo yangu,.,....
Mnamo mwaka 2004 nimaliza darasa la saba na baada ya hapo nilienda kusoma pre form one katika shule inayoitwa Don bosco seminary mafinga, maisha ya pale yalikuwa ni mazuri sana, kwani niliweza kupikwa vyema katika pande zote hususani ni kwa upande wa dini na masomo pia, nawakumbuka sana classmet zangu wote wa Don bosco seminary,
Nilipenda sana Music na Soka nikiwa don bosco seminary, kwani tuliweza kupata mda wa kukuza na kuonyesha vipaji vyetu, nakumbuka baadhi ya marafiki zangu walionifurahisha sana wakiimba ni kama Danstan kaganda (Boka) na Winfredy mgaya ( bozy), nawaombea muendeleze vipaji vyenu, lakini pia nawashukuru rafiki zangu ambao mara nyingi tuliweza kushauriana katika mambo mbalimbali kama osward lumato na Anthony frank, nawakumbuka sana classmet wangu wote wa Don bosco seminary na nawakubali sana
Nikiwa pale nilipenda sana kupiga kinanda na kucheza mpira,, vile vile nilipenda kuangalia soka na timu ninayoipenda ni manchester united
Mnamo mwaka 2009 nilimaliza masomo ya o-level na nikachaguliwa kwenda njombe secondary school,.
Huko nilienda kusoma form five na six, maisha yangu ya pale yalikuwa ni mazuri kabisa, japo kuwa katika kila mazuri hapakosi mabaya, hivyo pale napo nilipata mambo magumu hususani kwa upande wa masomo, masomo yalikuwa ni magumu na mambo yalikuwa ni mengi lakini nashukuru kwa kushirikiana na marafiki zangu nilifika salama
namshukuru sana rafiki au kaka yangu aloyce lyuvale kwa ushirikiano alionipa katika kafika malengo yango, lakini pia kuna walimu wangu walionisaidia sana advance ambao ni mwalimu ulime, meshack, shadrack n.k
pia nawashukuru watu wangu na marafiki zangu muhimu walinisaidia nakunipa companyi pale njombe kama agnes kidehele n.k
baada ya miaka miwili nilifanikiwa kumaliza na baada ya hapo nikachaguliwa kujiunga na sokoine university of agriculture kusomea Human nutrition, namshukuru Mumngu kwani nafurahia maisha ya sua na Morogoro kwa ujumla, hadi hivi sasa nipo hapa sua

No comments:
Post a Comment